Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote.
Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti.
Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zinazodorora kutokana na kubanwa na majukumu ya ukuu wa wilaya.
“Pamoja na ukuu wa wilaya, mimi pia ni mbunge na wakati huohuo ni mfanyabiashara; haya ni majukumu mengi kutekelezwa na mtu mmoja kwa wakati moja,” alisema Mayenga
Aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Nyamilangano, wilayani Ushetu kuwa biashara zake nyingi zilizopo mkoani Shinyanga zimedorora kutokana na kukosa usimamizi wake.
“Ombi hili nililitoa binafsi kwa Waziri Mkuu ambaye alinishauri kusubiri uteuzi; isitafsiriwe kwamba nimeogopa kasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano. Hapana! Nimeona ni vyema nibaki na ubunge na biashara zangu,” alisema Mayenga ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari.
Baadhi ya wanachama wa UWT waliohudhuria mkutano huo walimpongeza kwa uamuzi huo wakisema unapaswa kuigwa na viongozi wengine wenye majukumu mengi kwa kuachia watu wengine nafasi za kutumikia umma badala ya kung’ang’ania nafasi zote.
“Nampongeza Mheshimiwa Mayenga kwa uamuzi wake wa kuomba asiteuliwe tena kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya kwa sababu itatoa fursa kwa watu wengine kutumikia nafasi hiyo,” alisema Selina Mkula.
Katika mkutano huo ambao Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa alitoa msaada wa mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Nyamilangano na Mitonga pamoja na Shule ya Sekondari Kisuke, wanachama wapya 55 walijiunga na UWT.
Mbunge huyo pia aliahidi kutoa vyerehani 20 kwa makatibu kata wa UWT ili kusaidia harakati za maendeleo ya wananchi kwa kuanzisha vikundi vya kiuchumi katika kata zao.
Mwananchi
Mkuu wa Wilaya wa Iramba anyosha mikono na kumuomba Magufuli asimchague tena?
By Unknown
Kerry Washington participated in a talk about the New Rules of Social Stardom during the 2016 SXSW Music, Film + Interactive Festival at the Austin Convention Center on Sunday — and she addressed rumors that she and husband Nnamdi Asomugha are headed for divorce.
“I think — and this is something Reese Witherspoon has talked about a lot — it’s a little different for me because I don’t talk about my personal life,” said Kerry. “Social media has actually been great for [other celebrities’] relationships with the weeklies or the gossip sites because people say things and they say, ‘That’s not true! Just so you know, that’s BS!’ I say ‘BS’ because it’s Sunday. So I’m thinking in some ways, it’s been great because people are able to maintain their voice.”
“If I don’t talk about my personal life, it means I don’t talk about my personal life,” she continued. “That means not only did I not tell you when I was getting married, it also means if somebody has rumors about what’s going on in my marriage, I don’t refute them, because I don’t talk about my personal life.”
While that last bit has us giving Kerry a bit of a side-eye, she did refer to her husband when talking about being funny…so that’s a good sign. She joked:
“My husband says that I’m funnier since I became a mom, and that luckily I was pregnant when I did SNL because I was really funny. I think something about being a mom has made me let go even more of ideas of perfectionism, like when you’re pregnant you’re just not in control of anything. Like every day you’re like, ‘What am I today?’”
Well, if they’re happy — we’re happy.
Kerry Washington Addresses Rumors She’s Divorcing Husband Nnamdi Asomugha: ‘I Don’t Refute Them Because I Don’t Talk About My Personal Life’
By Unknown
Hatimaye rufaa ya wanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, imesikilizwa katika Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR) jijini Arusha Machi 11, mwaka huu na sasa zimebaki saa 72 tu kujua hatima yao, yaani Machi 18, 2016, UWAZI linakupa zaidi.
Rufaa hiyo ilisikilizwa na mahakama hiyo yenye majaji 11 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ambapo rais wao ni Jaji Augustine Ramadhani wa Tanzania ambaye pia aliwahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
MAJAJI WENYE SIRI MOYONI
Baadhi ya majaji waliotajwa kusikiliza rufaa hiyo na nchi zao kwenye mabano ni Ben Kioko (Kenya), Solomy Balungi Bassa (Uganda), Duncan Tambala (Malawi), Angelo Vasco Matuse (Msumbiji), Sylvain Ore (Ivory Coast), El Hadji Guisse (Senegal) na Rafaa Ben Achous (Tunisia).
KUTOKA MAHAKAMANI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka katika mahakama hiyo, rufaa hiyo ilisikilizwa kwa faragha na hakuna mwandishi wa habari yeyote aliyeruhusiwa kuingia kupata mwenendo.
Chanzo kilizidi kusema kuwa rufaa ya mwanamuziki huyo na mwanaye, ilisikilizwa kwa karibu saa tatu tangu ianze na matokeo au hukumu wanayo wahusika.
SABABU ZAFICHWA
Hata hivyo, si Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Ramadhani au mtu mwingine yeyote aliyeeleza sababu za kesi ya Babu Seya na mwanaye Papii Kocha isikilizwe faragha.
HATA JAJI RAMADHANI HAJUI
Wakati akichukua madaraka ya urais wa mahakama hiyo, Jaji Ramadhani alisema: “Kesi yoyote inayohusu nchi yangu mimi sitakiwi kuhudhuria kutokana na sheria zetu za mahakama hii…”
Kutokana na maneno hayo, kumezuka utata kwani haikujulikana mara moja kama wakati shauri la Babu Seya na mwanaye linasikilizwa, Jaji Ramadhani alikuwepo au la kwani rufaa ilipitiwa kwa faragha na kama alitoka nje basi itakuwa imepitiwa na majaji 10.
WATOA UAMUZI
Habari zaidi zinasema kuwa mara baada ya rufaa hiyo kupitiwa na majaji hao, shauri lao linapelekwa kwenye Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu ambako huko ndiko kutakakotolewa uamuzi ndani ya saa 72 zijazo.
WANACHODAI
Wanamuziki hao wamekata rufaa dhidi ya adhabu waliyohukumiwa mwaka 2004 ya kutumikia kifungo cha maisha jela ambapo mpaka sasa, wapo Gereza la Ukonga, Dar wakitumikia kifungo chao.
Kupitia shauri lao lililowasilishwa mahakamani na jalada lake kupewa namba 006/2015, wawili hao wanaiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi kuwa haki zao zilikiukwa na wanaomba waachiwe huru na kulipwa fidia.
Pia wanataka mahakama hiyo iteue wataalam watakaotoa ufafanuzi wa hoja za kesi yao na kuisaidia kufikia wajibu wake.
Miongoni mwa hoja za Babu Seya na mwanaye zilizosikilizwa mahakamani hapo, ni pamoja na kwamba mwenendo wa shauri lao haukufanyika kwa kuzingatia haki, vilevile wanadai hati ya mashitaka dhidi yao ilikosewa kuandikwa tarehe ambayo tuhuma za makosa yao zilidaiwa kufanywa hivyo wakashindwa kutayarisha utetezi wao.
Pia wanadai mahakama iliyowatia hatiani, ilijielekeza katika ushahidi wa upande wa mashitaka pekee usioshirikisha ushahidi mwingine.
WANAISEMA SERIKALI
Wanadai kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia maofisa wake, ilivunja misingi ya haki za binadamu na sheria za kimataifa kwani ilivunja Ibara 1, 2, 3, 5, 7(1) b, 13 na 18 (1) ya Mkataba wa Afrika wa Ubinadamu na Haki za Binadamu.
Wanadai kwamba mashitaka dhidi yao yalitungwa na hivyo hukumu iliyotolewa haikujikita katika ushahidi wenye nguvu katika sheria.
TUKUMBUSHANE
Oktoba 12, mwaka 2003, Nguza na wanaye watatu, Mbangu, Johnson na Francis walikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar wakidaiwa kubaka na kulawiti watoto 9, maeneo ya Sinza Palestina, Dar.
Oktoba 16, mwaka huohuo walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma hizo huku wakitetewa na Wakili Mabere Marando ambaye juzi hakupatikana alipotafutwa na gazeti hili ili kutoa ufafanuzi kupitia simu yake ya kiganjani.
Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye kwa hatia ya kubaka na kulawiti.
Januari 27, mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu dhidi yao.
Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao, Mabere Marando walikata rufaa ya pili ambayo ilitupiliwa mbali.
Mwaka 2010, waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari 2010. Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha huku ikiwaachia huru watoto wake, Mbangu na Francis.
Elvan Stambuli, UWAZI
Babu Seya na Papii kuachiwa huru ndani ya Saa 72?
By Unknown
Kajala Masanja mwenye umri wa miaka 33, anadaiwa kuwa na mahusiano Quick Rocka ambaye ana miaka 28.
Zuwena Mohammed ‘Shilole’ mwenye umri wa miaka 30, anatoka na msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Nedy Music mwenye umri wa miaka 20.
Vanessa Mdee ‘V-Money’ mwenye umri wa miaka 28 anasemekana kuwa anatoka na Juma Khalid ‘Jux’ ambaye naye ana umri wa miaka 28 lakini inasemekana Vanessa kamzidi JUX miezi kadhaa.
Riyama Ally ana umri wa miaka 30 lakini anadaiwa kuwa na mahusiano na Leo Mysterio mwenye umri wa miaka 26.
Aunt Ezekiel Grayson mwenye umri wa miaka 29 mzazi mwenziye Mose Iyobo ana umri wa miaka 23.
Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ aka Mama yake Tiffa ana umri wa miaka 35 ilihali mzazi mwenziye Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz ana umri wa miaka 26.
Umri sio kitu mapenzi ndio kila kitu ........
By Unknown
Subscribe to:
Posts (Atom)


















