DAR ES SALAAM: Siku 15 baada ya ndoa ya mwigizaji nyota, Wastara Juma na Mbunge wa Jimbo la Donge (CCM), Sadifa Juma kuvunjika, hali imekuwa tete kufuatia marafiki, jamaa na baadhi ya wasanii wa sinema za Bongo waliotoa michango yao kufanikisha sherehe ya ndoa (harusi) ya wawili hao kumtaka staa huyo kurudisha fedha zao, fuatana na Risasi Mchanganyiko.
Chanzo makini kilichokuwa karibu na kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo (jina lipo), kimeliambia gazeti hili kuwa, baadhi ya waliochanga fedha hizo wameanza kuulizia utaratibu wa kurudishiwa ‘mkwanja’ wao baada ya ndoa ya wawili hao waliodumu kwa siku 61 tu, kuparaganyika.
BONYEZA HAPA KUSIKIA CHANZO
“Yaani Wastara sijui ana matatizo gani! Wakati mwingine unaweza kukufuru na kusema ni mtu wa majanga. Ndoa imevunjika, sasa waliomchangia wanadai michango yao, kazi kwa dada yake Naima ambaye alikuwa mweka hazina.
“Kama walishalipia baadhi ya vitu unadhani itakuaje? Sherehe ilipangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa My Fair Plaza (jijini Dar) na najua hapa mjini huwezi kuupata ukumbi bila kulipa advance. Sijui kama watarudishiwa. Hapo ni pagumu kidogo.”
MASTAA WAFUNGUKA
Risasi Mchanganyiko liliwasaka baadhi ya mastaa walioshiriki vikao vya awali kwa sharti la kutotajwa majina yao, walisema ni vyema kama wangerudishiwa fedha zao kwa sababu lengo halijatimia.
“Mimi sioni sababu ya Wastara kuendelea kukaa na fedha zetu, arudishe tu. Si unajua siku hizi hali ni mbaya? Siyo rahisi kuiacha pesa ikaenda tu. Mimi nitamwambia Wastara, najua ataelewa,” alisema mmoja wa mastaa hao.
HUYU AMSHUKURU MUNGU
Mmoja wa mastaa hao, alimshukuru Mungu kwamba hakuchanga hata senti tano, kwani ahadi aliyotoa ilikuwa ni ya ‘mkwanja’ mrefu na hajui ingekuaje kama angeomba kurejeshewa.
SHOSTI WAKE AWEKA BAYANA
Naye rafiki wa karibu wa Wastara ambaye alikuwa mstari wa mbele kwa kila jambo, alisema pamoja na unafiki wa baadhi ya mastaa waliomchangia pesa, fedha hizo hazitarudishwa badala yake wataangalia kitu cha kufanya ili kutimiza azma iliyodhamiriwa.
“Mimi nawashangaa ambao wanadai kurudishiwa michango. Hivi mwenzetu yuko kwenye matatizo tunadai vipi pesa? Tungempa nafasi kwanza maana huwezi jua, hali inaweza kupoa na ndoa yao ikarudi kama kawa. Ile ni ndoa ya Kiislam bwana,” alisema rafiki huyo.
DADA WA WASTARA NA MWANAYE
Naima ni dada wa damu wa Wastara ambaye ni mweka hazina wa zoezi la uchangishaji fedha kwa shughuli hiyo. Gazeti hili lilimtafuta kupitia simu yake ya mkononi, lakini katika hali isiyotarajiwa, ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mwanaye.
Alipoulizwa sehemu alipo mama yake, badala ya kujibu, alitaka kufahamu chanzo cha mama yake kupigiwa simu na aliposomewa mashitaka ya mama yake, alisema hawezi kuongelea suala hilo hadi awepo mwenyewe ambapo hakusema sehemu alipo.
HUYU HAPA WASTARA MWENYEWE
Juhudi za kumtafuta Wastara ili kusikia anavyolizungumzia jambo hilo, naye hakuweza kupatikana, lakini kupitia kundi alilojiunga nalo katika Mtandao wa WhatsApp, gazeti hili lilinasa sauti yake akizungumzia ishu hiyo: “Asalam alaikum. Nawashukuru wote mlionipa moyo na kunizuia kuongea kuhusu ndoa yangu maana ningeongea mengi, lakini pia namshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema kwani mpaka sasa napumua. Ipo siku nitaongea mengi kabla sijaaga dunia.
“Nimemuomba dada yangu Leyla turudishe michango ya watu kwa sababu sipendi kuendelea kusemwa vibaya kama ninavyosikia. Tutahakikisha tumerudisha michango yote kwa kila aliyechanga.
“Hata hivyo, nawashukuru wote mlioandika ujumbe kuwa nisirudishe michango kwa vile mtaendelea na malengo mliyopanga. Kiukweli maneno yenu yamenipa faraja na nimeamini kuwa mnanipenda.”
TUMEFIKAJE HAPA?
Wastara na mumewe Sadifa Juma, walifunga ndoa miezi miwili iliyopita, tukio ambalo baadhi ya watu walio karibu, walisema ni mojawapo ya ndoa zitakazokabiliwa na changamoto kubwa, hasa baada ya kudaiwa kuwa jambo hilo lilifanywa kwa haraka isiyotarajiwa.
Tangu kufungwa kwa ndoa hiyo, kumekuwa na misuguano midogomidogo ya kawaida kujitokeza katika ndoa, kabla ya wiki mbili zilizopita zilipoibuka taarifa kuwa, wawili hao wamebwagana.
MTALAKA WAKE AMFUNGIA KAZI
Ijumaa iliyopita, mtalaka wa Wastara, Sadifa ndiyo alipanga kupeleka talaka nyumbani kwa staa huyo, Tabata, Dar. Akawachukua baadhi ya watu wake wa karibu, wakiwemo ndugu, tayari kwa safari.
“Lakini kabla hajawasha gari lake kwa ajili ya safari, aliona ni vyema akampigia simu dada yake Wastara, Naima kumwambia kwamba, anakwenda na talaka mkononi maana Wastara mwenyewe hayupo hapa mjini.
“Cha ajabu sasa, dada huyo alisema ametoka nyumbani. Kwa hiyo kama anapeleka talaka akamwachie mtu yeyote atakayemkuta,” kilisema chanzo hicho.
MTALAKA HUYU HAPA
Juzi, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Sadifa na kumuuliza kama alikumbana na hali hiyo ambapo alisema: “Mimi nilishawaambia Ijumaa nakwenda kupeleka talaka. Nilimpigia simu dada yake, akasema hayupo. Eti kama ni talaka nikamwachie yeyote. Sasa talaka utamwachiaje yeyote? Kwa hiyo sikwenda.”
No comments:
Post a Comment