Kama ulikosa kuangalia mahojiano ya Cloud na CHIDI BENZ angalia hapa

Fashenisto RIHANNA





LICHA ya kutumia nguvu nyingi kukanusha habari zinazochapishwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuwa, amerejea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amenaswa ‘laivu’ akiwa ‘ameangusha gari’ kando ya barabara, habari ndiyo hiyo!

Ray C ambaye kila anapoandikwa na Magazeti ya Global kuhusu kurejea kwenye unga, amekuwa akimtupia shutuma Mkurugenzi wa Global, Eric Shigongo kwamba anamchafua, alinaswa na mapaparazi wetu hivi karibuni maeneo ya Mwananyamala Magengeni, Dar akiwa amezima yeye na mwanaume aliyekuwa naye hali iliyompa urahisi paparazi wetu kuwafotoa picha za kutosha.

ISHU ILIANZA JANUARI
Januari mwaka huu, gazeti hili liliripoti habari iliyokuwa na kichwa: CHIMBO LA UNGA LA RAY C LAGUNDULIKA.

Baada ya habari hiyo kutoka, Ray C aliikanusha kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema: “Seriously kwa kweli huwa naumia sanasana kuona binadamu mwenzangu anadiriki kuniharibia jina langu ili yeye apate kula! Hamjui mnaniathiri kiasi gani na hizi habari zenu! Hiyo habari yaani ni ujingaujinga tu umeunganishwa na picha yangu bila hata uoga mmeichukua kutoka kwenye page yangu ya Insta. Mnazitumia kunichafulia jina langu tena wakati ndiyo kwanza nahangaika kurudi kwenye kazi yangu.”

TV ANDAGRAUNDI IKAMSAPOTI
Kama hiyo haitoshi, kituo kimoja cha runinga cha muda mrefu nchini lakini bado kiko ‘andagraundi’ kilimpa nafasi Ray C akanushe habari ya Ijumaa Wikienda pasipo kujua gazeti hili lilijiridhisha kabla ya kuandika habari hiyo.

SHIGONGO ATAKA UKWELI
Baada ya Ray C kuyaponda Magazeti ya Global kwenye runinga kwa kudai yanamchafua, Shigongo alimuagiza Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Oscar Ndauka kupanga makachero kutokea kwenye kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ili kufuatilia nyendo za msanii huyo kama kweli anaonewa au la na kutaka matokeo yaliyo kamili!

OFM KAZINI
Timu ya OFM ilipangwa kwa zamu kumfuatilia Ray C kwa saa ishirini na nne ili kujiridhisha juu ya malalamiko yake, hasa kwamba Global inaungaunga picha za zamani ili kupata habari kama alivyosema kwenye Instagram yake.

Tangu Januari hiyo, timu ya OFM ilianza kuwa sambamba na Ray C huku makachero wengine wakiwasaka watu wake wa karibu ili kusikia chochote kutoka kwao.

MSIKIE HUYU
“Mimi ni miongoni mwa watumiaji wa madawa ya kulevya ambaye nilishawishiwa na Ray C kuacha na kunileta hapa kwenye Kituo cha Mwanayamala (hospitali) kwa ajili ya kuanza kumeza Methadone (dawa za kuponya waathirika wa madawa ya kulevya) ili niweze kurudia hali yangu ya kawaida. Hali yangu sasa niko safi na najitambua. AMSIKITIKIA

RAY C
“Kinachoniuma ni Ray C ambaye aliniunganisha hospitali kwa mbwembwe, yeye ameshindwa kuendelea na kapata bwana ambaye amemsaidia kurudia tena matumizi ya unga kushinda zamani. Huwezi amini kwa sasa mwenzetu gari limewaka upya, anawasumbua hata madaktari wetu, wakati mwingine wamekuwa wakishindwa kumhudumia.

FULL VURUGU
“Akija hapa kituoni kuchukua dawa muda wote ni kuwasimanga hawa wauguzi wetu jambo ambalo linatukera sana kwani anatuharibia hata sisi ambao alituleta. Aliyemponza ni Frank. Frank alikuja hapa kituoni kama mwathirika na kuanza kutumia dawa.

“Baada ya kukutana na Ray C na kuwa marafiki, wameshindwa kuendelea kutumia dawa. Badala yake wamekuwa wakivuta unga kiasi cha kuzima na kuleta fujo tu. Huyu Frank anaishi Mwananyamala karibu na hapa hospitali,” alisema mwathirika mmoja akiomba kufichiwa jina lake.

MADAKTARI WALIMSUSA
Akaendelea: “Unajua  madaktari wa hapa  walifikia hatua ya kujivua kumhudumia na kumrejesha kwao kipindi kile alipofanya fujo Posta. Ninasema haya kwa uchungu maana hata sisi tunaokunywa naye dawa hakuna hata mmoja anayeweza kummudu zaidi ya huyo Frank ambaye naye gari limeshachanganya, anampoteza kabisa Ray C,” kilisema chanzo hicho.”

JK ANYOOSHA MIKONO, AMUACHIA MAGUFULI
Chanzo kingine kilichopo kwenye hospitali hiyo kililiambia Ijumaa Wikienda kuwa, kutokana na JK kumsaidia alipokuwa madarakani na mrembo huyo kurejea tena kwenye unga, amenyoosha mikono, jukumu hilo litabaki kwa rais wa sasa, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’.

“JK ameshanyoosha mikono. Hawezi tena kumuelewa huyu dada, amemuachia Magufuli naye labda ajaribu kwani ndiye aliyeko madarakani,” kilisema chanzo hicho.

RAY C MWENYEWE HUYU HAPA
Alipotafutwa Ray C juzi na kusomewa madai hayo na kuelezwa juu ya kupigwa picha zinazomuonesha akiwa amezima, alifunguka: “Kweli kuna picha nimesikia watu walinipiga nikiwa nimezimika lakini siyo kwamba nilivuta unga kiasi hicho, picha hizo nilipigwa kweli nikiwa nimezima baada ya kunywa dawa hapo hospitali maana dawa ninazokunywa huwa ni kali sana, saa nyingine huwa nashindwa kujizuia na kujikuta nimezima.
“Kwanza unatakiwa ujue kwamba hizi dawa siku zote ukinywa hata kama ungekuwa na nguvu kiasi gani lazima kuna muda unafikia hatua ya kushindwa kabisa kujimudu na saa nyingine huwa tunalala hata na wenzangu kwani hata hizo picha wamenipiga chini ya mti hapahapa jirani na eneo la hospitali, siku hiyo nilikuwa nimezidiwa sana.”

AMTAJA FRANK KAMA ‘BEBI’ WAKE
“Ninachokijua nilala chini ya mti na Frank lakini hata ukiangalia nyuma yetu pia
kuna watu kibao ambao nao walikuwa wamelala baada ya kunywa dawa na kuzidiwa, sasa sijui wewe hizo zangu na huyo mpenzi wangu umezitoa wapi,” alisema Ray C.

DAKTARI WA WAATHIRIKA AZUNGUMZA
Baada ya utetezi huo wa Ray C, gazeti hili lilimwendea hewani daktari wa tiba kwa waathirika na unga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo) na kumuuliza kama matumizi ya dawa za Methadone yanaweza kumzimisha mtumiaji ambapo alisema:
“Kama anayetumia Methadone baada ya kuathirika hatatumia madawa ya kulevya hawezi kuzima kwa namna yoyote ile. Ukimwona mtu anazima ujue anachanganya, yaani anameza Methadone pia anaendelea kubwia unga.”

TUMEFIKAJE HAPA?
Ray C aliyewahi kutamba na nyimbo nyingi kali, ikiwemo Na Wewe Milele, alijikuta ametopea kwenye madawa ya kulevya baada ya kutumbukia kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa staa wa Hip Hop Bongo, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ ambaye naye anadaiwa kutumia.

Baadaye wawili hao walimwagana huku Ray C akichanja mbuga katika eneo hilo hali iliyomlazimisha ‘kustaafu’ muziki kutokana na mwili kukosa mawasiliano katika kupanga mikakati.

Gazeti damu moja na hili, Ijumaa, toleo Namba 799 la Novemba 2-8, 2012 lilitoa picha za Ray C akiwa amezimika na habari yenye kichwa; DAH!
RAY C. Tukio hilo lilijiri maeneo ya Magomeni, Dar.

JK ASOMA, APATA UCHUNGU
Wiki moja baada ya gazeti hilo kuingia mtaani likielezea hali ya Ray C, JK alimwita Ikulu ya Dar es Salaam yeye, mama yake mzazi, Margaret Mtweve na ndugu mwingine hali iliyoonesha kuwa, aliisoma habari hiyo kwenye Gazeti la Ijumaa.

Lengo la kumwita lilikuwa kumsaidia mwanamuziki huyo kwa tiba na uangalizi wa kina jambo ambalo lilifanyika na akarudia kwenye hali yake ya kawaida.

Mwaka 2015, baada ya minong’ono mingi kwamba msanii huyo amerejea katika matumizi ya unga, magazeti ya Global yaliandika habari hiyo na Ray C akawa anakanusha mara kwa mara mpaka majuzi aliponaswa akiwa amezima.

Musa Mateja, Wikienda

RAY C na kashfa ya kubwia unga tena?

Bridesmaids photos



 


Kufuru! Ndilo neno pekee linaloweza kuakisi takriban Sh. milioni 100 ambazo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameziteketeza akiwa na msururu mrefu wa wanafamilia wa Wasafi Classic Baby (WCB) barani Ulaya, akianzia nchini Ujerumani kufanya shoo sambamba na kula bata, Wikienda linakupa habari kamili.

Diamond aliyeambatana na wanafamilia kama 14 wakiwemo Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, Tiffah (mwanaye), Romy Jons (DJ wake), Kifesi (mpigapicha), meneja (Salam), mke wa Tale (meneja Tale), madansa wanne na dada mmoja ambaye ni ndugu wa Zari, walikwea pipa na kufikia Frankfurt, Ujerumani.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo kilicho karibu na familia ya Diamond kilichoambatana na msafara huo kilipenyeza ‘ubuyu’ kuwa, kwa kushirikiana na uongozi wake, Diamond alitenga si chini ya Sh. milioni 100 ili kufanikisha ziara hiyo aliyoipa jina la Europe Tour ambapo inatarajiwa kuchukua takriban wiki tatu.

“Diamond ni noma, ameandaa mkwanja usiopungua milioni 100 kwa ajili ya msafara wake. Fedha hizo zitatumika kuanzia usafiri wa ndege kwenda na kurudi, chakula, shopping na malazi kwa kipindi chote cha wiki tatu atakachokuwa Ulaya,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

WATUA FRANKFURT
“Walitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Frankfurt, Ijumaa (iliyopita), walichelewa kutoka uwanja wa ndege kwa sababu walikuwa na mizigo mingi lakini pia bahati mbaya kitoroli cha kumbebea Tiffah kilipotea hivyo uongozi ulichukua muda mrefu kukitafuta hadi walipokipata.”

AMEFUATA NINI NCHINI HUMO?
Chanzo hicho kiling’amua kuwa, Diamond alikuwa na ziara ya kimuziki barani Ulaya lakini kwa kuwa imeangukia wakati wa Sikukuu ya Pasaka, aliamua kuambatana na mama yake, mpenzi wake (Zari) na mwanaye ili wakainjoi.

“Ameona aitumie ziara hii ya kimuziki pia kuinjoi. Kila atakapokuwa anapita atakuwa anapata muda wa kula bata za nguvu, kufanya shopping za hapa na pale ambapo kama unavyojua tena huyu Diamond ndiyo Rais wa Wasafi, kila anapotua na msafara mzima unalala kwenye hoteli ya kifahari ambayo si chini ya nyota tatu.

SHOO ZOTE HIZI HAPA
“Jumamosi (iliyopita) ndiyo ataanza kupiga shoo Franfurt, Machi 25, atakuwa Oslo (Norway), Machi 26, atakuwa Bergen (Norway), Machi 27, atakuwa Stockholm (Sweden), Aprili 1, atakuwa Bruxelles (Belgium), Aprili 2 ni Stuttgart (Ujerumani), Aprili 8 ni Helsink (Finland) na Aprili 9 atamalizia Copenhagen (Denmark),” kilisema chanzo hicho.

SHOO ZITAFIDIA MATUMIZI?
Ijumaa Wikienda lilipokibana chanzo hicho kutaka kujua Diamond ataingiza shilingi ngapi kama malipo ya shoo hizo ili kufidia au kuzidi matumizi ya shilingi milioni 100, kilisema hakina uhakika wa malipo ya shoo kama yatafidia gharama lakini kikashauri aulizwe Diamond mwenyewe.
“Dah! Kuhusu malipo ya shoo, mimi kwa kweli sijui japo naamini lazima itamlipa, Diamond siyo mpuuzi aje huku atumie hela nyingi kuliko fedha atakazolipwa kwenye shoo. Wote atupandishe ndege daraja la kati. Atakuwa ameshafanya hesabu na kuona anabaki na faida katika ziara ndiyo maana akakubali kuja na msafara mkubwa, ila kama vipi muulize mwenyewe,” kilisema chanzo hicho.

DIAMOND HUYU HAPA
Wikienda lilimtafuta Diamond kupitia Mtandao wa WhatsApp ili kutaka alithibitishe ukweli wa yeye kuteketeza shilingi milioni 100 katika ziara hiyo ambapo alikataa kuzungumzia malipo aliyoyapata kwa shoo hizo lakini akadai kuwa zinaweza kufika au hata zaidi kulingana na starehe watakazoamua kuzifanya.

“Siwezi kusema moja kwa moja kama inafika au la lakini inaweza kufika na hata zaidi. Wewe chukulia mimi tu na familia yangu (yeye, Tiffah, Zari na ndugu zake) nimetenga kama dola 30,000 (zaidi ya Sh. milioni 65) kwa ajili ya usafiri, malazi na shopping za hapa na pale sasa vipi kuhusu timu nzima ya madansa, meneja na wengine?” alihoji Diamond.

UCHUNGUZI WA WIKIENDA
Gazeti hili lilifanya uchunguzi wa wastani wa bei ya nauli pekee kutoka Bongo hadi Ujerumani kwa daraja la chini (Economy Class) si chini ya shilingi milioni 3 kwa mtu mmoja. Daraja la kati (Business Class) si chini ya shilingi milioni 5 kwa mtu mmoja kwa maana ya kwenda na kurudi Bongo.

MCHANGANUO ZAIDI
Kama wamepanda watu wote (14) kwenye Economy Class maana yake watakuwa wametumia si chini ya Sh. milioni 42 kwa usafiri pekee. Lakini endapo watakuwa wamepanda Business Class watakuwa wametumia si chini ya Sh. milioni 70.

INAWEZEKANA!
Kama familia ya Diamond imetumia Sh. milioni 65 kwa malazi, usafiri na shopping ni zaidi ya robo tatu ya Sh. milioni 100 hivyo ni dhahiri timu iliyosalia inaweza kuwa imetumia zaidi ya Sh. milioni 30 kwa nauli, malazi na chakula, jambo ambalo halijawahi kutokea Bongo kwa staa yeyote.

Habari GPL
Picha : Kwa msaada wa Mtandao

Tumia hela ikuzoee... DIAMOND afanya kufuru ULAYA angalia baadhi ya picha zao hapa




Former basketball pro Lamar attended church with Khloe and sister Kourtney and Kendall

He was left fighting for his life after collapsing in a brothel just five months ago.

But Lamar Odom looked the picture of health as he joined his ex Khloe Kardashian for an Easter church service.

The former NBA pro joined Khloe and the rest of her family at a service in Agoura Hills, California today.

Lamar held hands with Mason Disick, the son of Kourtney Kardashian, as the group made their way into the church.

The star was dressed in a grey hooded sweatshirt, black jeans and trainers while Khloe, who he is still legally married to, looked glamorous in a white trouser suit with a white trilby hat.

Keeping Up With the Kardashians star Khloe, 31, remained by Lamar's side through his health battles and called off their divorce last year so she could continue making medical decisions on his behalf.

She recently opened up about the importance of staying friends with her exes , saying: "If it's a relationship that served a purpose in my life, like Lamar, why wouldn't I want them in my life afterwards?"

Khloe's sister Kourtney also attended the service and went to the church in a see-through white top which flashed her bra.

She teamed her racy top with a pair of wide-legged white trousers and held her son Reign in her arms.

Model Kendall Jenner followed close behind dressed in a pair of cropped blue jeans with rips in the knees, a flowing blue top which flashed her navel, and silver sandals.

Momager Kris Jenner was also there with her boyfriend Corey Gamble.

Mirror

Lamar Odom looks happy and healthy as he joins Khloe Kardashian for Easter service


Dar es Salaam: Hatimaye! Taarifa ikufikie kwamba, staa wa kitambo wa Bongo Muvi, Riyama Ally amelipiwa mahari na mpenzi wake ‘sharobaro’ ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Haji  Mwalimu ‘Leo Mysterio’ huku mipango kabambe ya ndoa ikiendelea.

Riyama ameliambia Wikienda kuwa, anamshukuru Mungu kumpata mtu anayeona ndiye anamfaa katika maisha yake na tayari sasa ni mchumba rasmi wa mtu, tena kijana anayempenda kwa dhati.

“Sasa hapa ndiyo nimefika kwa kuwa nimekutana na mtu mwenye mapenzi ya kweli kwangu. Pia nafsi zetu zimeendana, hapa namuomba Mungu anyooshe mambo yaende kama vile tulivyopanga,” alisema Riyama ambaye amekuwa ‘singo’ kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, Mysterio alisema kuwa anaamini safari yake ya muda mrefu imefika kwa kuwa amempata mwanamke anayempenda kutoka ndani ya uvungu wa moyo wake na kwa upande wake taratibu zote za uchumba amemaliza, anasubiri ndoa watakayofunga hivi karibuni.

Na Imelda Mtema, Wikienda

Hatimaje RIYAMA atolewa , sasa ni mchumba rasmi wa SHAROBARO

Romantic Honeymoon bedrooms


Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote.

Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti.

Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zinazodorora kutokana na kubanwa na majukumu ya ukuu wa wilaya.

“Pamoja na ukuu wa wilaya, mimi pia ni mbunge na wakati huohuo ni mfanyabiashara; haya ni majukumu mengi kutekelezwa na mtu mmoja kwa wakati moja,” alisema Mayenga

Aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Nyamilangano, wilayani Ushetu kuwa biashara zake nyingi zilizopo mkoani Shinyanga zimedorora kutokana na kukosa usimamizi wake.

“Ombi hili nililitoa binafsi kwa Waziri Mkuu ambaye alinishauri kusubiri uteuzi; isitafsiriwe kwamba nimeogopa kasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano. Hapana! Nimeona ni vyema nibaki na ubunge na biashara zangu,” alisema Mayenga ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari.

Baadhi ya wanachama wa UWT waliohudhuria mkutano huo walimpongeza kwa uamuzi huo wakisema unapaswa kuigwa na viongozi wengine wenye majukumu mengi kwa kuachia watu wengine nafasi za kutumikia umma badala ya kung’ang’ania nafasi zote.

“Nampongeza Mheshimiwa Mayenga kwa uamuzi wake wa kuomba asiteuliwe tena kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya kwa sababu itatoa fursa kwa watu wengine kutumikia nafasi hiyo,” alisema Selina Mkula.

Katika mkutano huo ambao Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa alitoa msaada wa mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Nyamilangano na Mitonga pamoja na Shule ya Sekondari Kisuke, wanachama wapya 55 walijiunga na UWT.

Mbunge huyo pia aliahidi kutoa vyerehani 20 kwa makatibu kata wa UWT ili kusaidia harakati za maendeleo ya wananchi kwa kuanzisha vikundi vya kiuchumi katika kata zao.

Mwananchi

Mkuu wa Wilaya wa Iramba anyosha mikono na kumuomba Magufuli asimchague tena?


Kerry Washington participated in a talk about the New Rules of Social Stardom during the 2016 SXSW Music, Film + Interactive Festival at the Austin Convention Center on Sunday  — and she addressed rumors that she and husband Nnamdi Asomugha are headed for divorce.

“I think — and this is something Reese Witherspoon has talked about a lot — it’s a little different for me because I don’t talk about my personal life,” said Kerry. “Social media has actually been great for [other celebrities’] relationships with the weeklies or the gossip sites because people say things and they say, ‘That’s not true! Just so you know, that’s BS!’ I say ‘BS’ because it’s Sunday. So I’m thinking in some ways, it’s been great because people are able to maintain their voice.”

“If I don’t talk about my personal life, it means I don’t talk about my personal life,” she continued. “That means not only did I not tell you when I was getting married, it also means if somebody has rumors about what’s going on in my marriage, I don’t refute them, because I don’t talk about my personal life.”

While that last bit has us giving Kerry a bit of a side-eye, she did refer to her husband when talking about being funny…so that’s a good sign. She joked:

“My husband says that I’m funnier since I became a mom, and that luckily I was pregnant when I did SNL because I was really funny. I think something about being a mom has made me let go even more of ideas of perfectionism, like when you’re pregnant you’re just not in control of anything. Like every day you’re like, ‘What am I today?’”

Well, if they’re happy — we’re happy.

Kerry Washington Addresses Rumors She’s Divorcing Husband Nnamdi Asomugha: ‘I Don’t Refute Them Because I Don’t Talk About My Personal Life’


Hatimaye rufaa ya wanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, imesikilizwa katika Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR) jijini Arusha Machi 11, mwaka huu na sasa zimebaki saa 72 tu kujua hatima yao, yaani Machi 18, 2016, UWAZI linakupa zaidi.

Rufaa hiyo ilisikilizwa na mahakama hiyo yenye majaji 11 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ambapo rais wao ni Jaji Augustine Ramadhani wa Tanzania ambaye pia aliwahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

MAJAJI WENYE SIRI MOYONI
Baadhi ya majaji waliotajwa kusikiliza rufaa hiyo na nchi zao kwenye mabano ni Ben Kioko (Kenya), Solomy Balungi Bassa (Uganda), Duncan Tambala (Malawi), Angelo Vasco Matuse (Msumbiji), Sylvain Ore (Ivory Coast), El Hadji Guisse (Senegal) na Rafaa Ben Achous (Tunisia).

KUTOKA MAHAKAMANI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka katika mahakama hiyo, rufaa hiyo ilisikilizwa kwa faragha na hakuna mwandishi wa habari yeyote aliyeruhusiwa kuingia kupata mwenendo.

Chanzo kilizidi kusema kuwa rufaa ya mwanamuziki huyo na mwanaye, ilisikilizwa kwa karibu saa tatu tangu ianze na matokeo au hukumu wanayo wahusika.

SABABU ZAFICHWA
Hata hivyo, si Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Ramadhani au mtu mwingine yeyote aliyeeleza sababu za kesi ya Babu Seya na mwanaye Papii Kocha isikilizwe faragha.

HATA JAJI RAMADHANI HAJUI
Wakati akichukua madaraka ya urais wa mahakama hiyo, Jaji Ramadhani alisema: “Kesi yoyote inayohusu nchi yangu mimi sitakiwi kuhudhuria kutokana na sheria zetu za mahakama hii…”

Kutokana na maneno hayo, kumezuka utata kwani haikujulikana mara moja kama wakati shauri la Babu Seya na mwanaye linasikilizwa, Jaji Ramadhani alikuwepo au la kwani rufaa ilipitiwa kwa faragha na kama alitoka nje basi itakuwa imepitiwa na majaji 10.

WATOA UAMUZI
Habari zaidi zinasema kuwa mara baada ya rufaa hiyo kupitiwa na majaji hao, shauri lao linapelekwa kwenye Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu ambako huko ndiko kutakakotolewa uamuzi ndani ya saa 72 zijazo.

WANACHODAI
Wanamuziki hao wamekata rufaa dhidi ya adhabu waliyohukumiwa mwaka 2004 ya kutumikia kifungo cha maisha jela ambapo mpaka sasa, wapo Gereza la Ukonga, Dar wakitumikia kifungo chao.

Kupitia shauri lao lililowasilishwa mahakamani na jalada lake kupewa namba 006/2015, wawili hao wanaiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi kuwa haki zao zilikiukwa na wanaomba waachiwe huru na kulipwa fidia.

Pia wanataka mahakama hiyo iteue wataalam watakaotoa ufafanuzi wa hoja za kesi yao na kuisaidia kufikia wajibu wake.

Miongoni mwa hoja za Babu Seya na mwanaye zilizosikilizwa mahakamani hapo, ni pamoja na kwamba mwenendo wa shauri lao haukufanyika kwa kuzingatia haki, vilevile wanadai hati ya mashitaka dhidi yao ilikosewa kuandikwa tarehe ambayo tuhuma za makosa yao zilidaiwa kufanywa hivyo wakashindwa kutayarisha utetezi wao.

Pia wanadai mahakama iliyowatia hatiani, ilijielekeza katika ushahidi wa upande wa mashitaka pekee usioshirikisha ushahidi mwingine.

WANAISEMA SERIKALI
Wanadai kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia maofisa wake, ilivunja misingi ya haki za binadamu na sheria za kimataifa kwani ilivunja Ibara 1, 2, 3, 5, 7(1) b, 13 na 18 (1) ya Mkataba wa Afrika wa Ubinadamu na Haki za Binadamu.

Wanadai kwamba mashitaka dhidi yao yalitungwa na hivyo hukumu iliyotolewa haikujikita katika ushahidi wenye nguvu katika sheria.

TUKUMBUSHANE
Oktoba 12, mwaka 2003, Nguza na wanaye watatu, Mbangu, Johnson na Francis walikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar wakidaiwa kubaka na kulawiti watoto 9, maeneo ya Sinza Palestina, Dar.

Oktoba 16, mwaka huohuo walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma hizo huku wakitetewa na Wakili Mabere Marando ambaye juzi hakupatikana alipotafutwa na gazeti hili ili kutoa ufafanuzi kupitia simu yake ya kiganjani.

Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye kwa hatia ya kubaka na kulawiti.

Januari 27, mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu dhidi yao.

Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao, Mabere Marando walikata rufaa ya pili ambayo ilitupiliwa mbali.

Mwaka 2010, waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari 2010. Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha huku ikiwaachia huru watoto wake, Mbangu na Francis.

Elvan Stambuli, UWAZI

Babu Seya na Papii kuachiwa huru ndani ya Saa 72?

Kajala Masanja mwenye umri wa miaka 33, anadaiwa kuwa na mahusiano  Quick Rocka ambaye ana miaka 28.

Zuwena Mohammed ‘Shilole’ mwenye umri wa miaka 30, anatoka na msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Nedy Music mwenye umri wa miaka 20.

 Vanessa Mdee ‘V-Money’ mwenye umri wa miaka 28 anasemekana kuwa anatoka na Juma Khalid ‘Jux’ ambaye naye ana umri wa miaka 28 lakini  inasemekana Vanessa kamzidi  JUX  miezi kadhaa.

 
Riyama Ally ana umri wa miaka 30 lakini anadaiwa kuwa na mahusiano  na Leo Mysterio mwenye umri wa miaka 26.

Aunt Ezekiel Grayson mwenye umri wa miaka 29  mzazi mwenziye Mose Iyobo ana umri wa miaka 23.

Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’  aka Mama yake Tiffa ana  umri wa miaka 35 ilihali mzazi mwenziye Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz  ana umri wa miaka 26.

Umri sio kitu mapenzi ndio kila kitu ........

Daphne Joy in Casa Aramara, Punta Mita

 Daphne Joy is red hot in a sexy two-piece

  Daphne catches some rays on the beach

She knows how to handle a surfboard

Jason Derulo's stunning girlfriend Daphne Joy is red hot in cut-out busty bikini on the beach