DAR ES SALAAM: Siku 15 baada ya ndoa ya mwigizaji nyota, Wastara Juma na Mbunge wa Jimbo la Donge (CCM), Sadifa Juma kuvunjika, hali imekuwa tete kufuatia marafiki, jamaa na baadhi ya wasanii wa sinema za Bongo waliotoa michango yao kufanikisha sherehe ya ndoa (harusi) ya wawili hao kumtaka staa huyo kurudisha fedha zao, fuatana na Risasi Mchanganyiko.

Chanzo makini kilichokuwa karibu na kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo (jina lipo), kimeliambia gazeti hili kuwa, baadhi ya waliochanga fedha hizo wameanza kuulizia utaratibu wa kurudishiwa ‘mkwanja’ wao baada ya ndoa ya wawili hao waliodumu kwa siku 61 tu, kuparaganyika.

BONYEZA HAPA KUSIKIA CHANZO
“Yaani Wastara sijui ana matatizo gani! Wakati mwingine unaweza kukufuru na kusema ni mtu wa majanga. Ndoa imevunjika, sasa waliomchangia wanadai michango yao, kazi kwa dada yake Naima ambaye alikuwa mweka hazina.

“Kama walishalipia baadhi ya vitu unadhani itakuaje? Sherehe ilipangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa My Fair Plaza (jijini Dar) na najua hapa mjini huwezi kuupata ukumbi bila kulipa advance. Sijui kama watarudishiwa. Hapo ni pagumu kidogo.”

MASTAA WAFUNGUKA
Risasi Mchanganyiko liliwasaka baadhi ya mastaa walioshiriki vikao vya awali kwa sharti la kutotajwa majina yao, walisema ni vyema kama wangerudishiwa fedha zao kwa sababu lengo halijatimia.

“Mimi sioni sababu ya Wastara kuendelea kukaa na fedha zetu, arudishe tu. Si unajua siku hizi hali ni mbaya? Siyo rahisi kuiacha pesa ikaenda tu. Mimi nitamwambia Wastara, najua ataelewa,” alisema mmoja wa mastaa hao.

HUYU AMSHUKURU MUNGU
Mmoja wa mastaa hao, alimshukuru Mungu kwamba hakuchanga hata senti tano, kwani ahadi aliyotoa ilikuwa ni ya ‘mkwanja’ mrefu na hajui ingekuaje kama angeomba kurejeshewa.

SHOSTI WAKE AWEKA BAYANA
Naye rafiki wa karibu wa Wastara ambaye alikuwa mstari wa mbele kwa kila jambo, alisema pamoja na unafiki wa baadhi ya mastaa waliomchangia pesa, fedha hizo hazitarudishwa badala yake wataangalia kitu cha kufanya ili kutimiza azma iliyodhamiriwa.

“Mimi nawashangaa ambao wanadai kurudishiwa michango. Hivi mwenzetu yuko kwenye matatizo tunadai vipi pesa? Tungempa nafasi kwanza maana huwezi jua, hali inaweza kupoa na ndoa yao ikarudi kama kawa. Ile ni ndoa ya Kiislam bwana,” alisema rafiki huyo.

DADA WA WASTARA NA MWANAYE
Naima ni dada wa damu wa Wastara ambaye ni mweka hazina wa zoezi la uchangishaji fedha kwa shughuli hiyo. Gazeti hili lilimtafuta kupitia simu yake ya mkononi, lakini katika hali isiyotarajiwa, ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mwanaye.

Alipoulizwa sehemu alipo mama yake, badala ya kujibu, alitaka kufahamu chanzo cha mama yake kupigiwa simu na aliposomewa mashitaka ya mama yake, alisema hawezi kuongelea suala hilo hadi awepo mwenyewe ambapo hakusema sehemu alipo.

HUYU HAPA WASTARA MWENYEWE
Juhudi za kumtafuta Wastara ili kusikia anavyolizungumzia jambo hilo, naye hakuweza kupatikana, lakini kupitia kundi alilojiunga nalo katika Mtandao wa WhatsApp, gazeti hili lilinasa sauti yake akizungumzia ishu hiyo: “Asalam alaikum. Nawashukuru wote mlionipa moyo na kunizuia kuongea kuhusu ndoa yangu maana ningeongea mengi, lakini pia namshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema kwani mpaka sasa napumua. Ipo siku nitaongea mengi kabla sijaaga dunia.

“Nimemuomba dada yangu Leyla turudishe michango ya watu kwa sababu sipendi kuendelea kusemwa vibaya kama ninavyosikia. Tutahakikisha tumerudisha michango yote kwa kila aliyechanga.

“Hata hivyo, nawashukuru wote mlioandika ujumbe kuwa nisirudishe michango kwa vile mtaendelea na malengo mliyopanga. Kiukweli maneno yenu yamenipa faraja na nimeamini kuwa mnanipenda.”

TUMEFIKAJE HAPA?
Wastara na mumewe Sadifa Juma, walifunga ndoa miezi miwili iliyopita, tukio ambalo baadhi ya watu walio karibu, walisema ni mojawapo ya ndoa zitakazokabiliwa na changamoto kubwa, hasa baada ya kudaiwa kuwa jambo hilo lilifanywa kwa haraka isiyotarajiwa.

Tangu kufungwa kwa ndoa hiyo, kumekuwa na misuguano midogomidogo ya kawaida kujitokeza katika ndoa, kabla ya wiki mbili zilizopita zilipoibuka taarifa kuwa, wawili hao wamebwagana.

MTALAKA WAKE AMFUNGIA KAZI
Ijumaa iliyopita, mtalaka wa Wastara, Sadifa ndiyo alipanga kupeleka talaka nyumbani kwa staa huyo, Tabata, Dar. Akawachukua baadhi ya watu wake wa karibu, wakiwemo ndugu, tayari kwa safari.

“Lakini kabla hajawasha gari lake kwa ajili ya safari, aliona ni vyema akampigia simu dada yake Wastara, Naima kumwambia kwamba, anakwenda na talaka mkononi maana Wastara mwenyewe hayupo hapa mjini.

“Cha ajabu sasa, dada huyo alisema ametoka nyumbani. Kwa hiyo kama anapeleka talaka akamwachie mtu yeyote atakayemkuta,” kilisema chanzo hicho.

MTALAKA HUYU HAPA
Juzi, Risasi Mchanganyiko  lilimpigia simu Sadifa na kumuuliza kama alikumbana na hali hiyo ambapo alisema: Mimi nilishawaambia Ijumaa nakwenda kupeleka talaka. Nilimpigia simu dada yake, akasema hayupo. Eti kama ni talaka nikamwachie yeyote. Sasa talaka utamwachiaje yeyote? Kwa hiyo sikwenda.”

Baada ya WASTARA kuachika watu wadi michango yao ya Harusi!


Right now, rap boogeyman and former Death Row Records CEO is in jail, facing a possible life sentence after he killed a man in a hit-and-run on the set of the movie Straight Outta Compton. As Pitchfork reports, Knight, for reasons unknown, has been denied the privileges of phone access and of receiving visitors other than his attorneys. And part of an effort to get his privileges restored, Knight’s lawyer has claimed that Knight is being silenced to prevent him from telling of how his old associate Dr. Dre hired a hitman to kill him.

Knight was wounded in a 2014 nightclub shooting, and according to his lawyer Thaddeus Culpepper, a police officer told Knight that a man named Tee-Money had confessed to the shooting. This Tee-Money allegedly claimed that Dre had paid him and a friend to kill Knight. Culpepper also claims that there’s video of off-duty police helping the hitmen to enter and escape the club, and that police “inexplicably released Tee-Money.”

A lawyer for Dre tells TMZ that Knight’s claim is “ridiculous.”

Suge Knight Says Dr. Dre Hired A Hitman To Kill Him

Davido wa sasa



   

Angalia picha za DAVIDO kabla hawaja maarufu

 Mwisho mwampamba kortini

 Robert Ephraim Mwampamba anayedaiwa kumbuluza Mwisho mahakamani.

Akiwa kwenye gari la polisi.

MOROGORO: Ikiwa takriban siku 40 tangu baba yao, Dk. Ephraim Njawala Mwampamba, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) afariki dunia, mwanaye Mwisho Ephraim Mwampamba ameburuzwa mahakamani na kaka yake, Robert Ephraim Mwampamba, Jumatatu iliyopita.

Kesi hiyo namba 197/2016 ilisikilizwa katika  Mahakama ya Mwanzo Chamwino iliyopo Mazimbu mkoani hapa, ambapo Robert alimburuza mahakamani hapo mdogo wake huyo waliyechangia baba, akimtuhumu kumtukana matusi ya nguoni huku sehemu kubwa ya matusi hayo yakiwa ya kibaguzi.

Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Mwisho alitokea mahabusu alikolala kwa siku moja ambapo baada ya kesi kusikilizwa, alipata dhamana huku ikidaiwa kuwa kesi hiyo imemkalia vibaya kutokana na ushahidi unadaiwa upo.

Akisoma kesi hiyo mahakamani hapo, Hakimu Amina Chungulu alidai Mwisho anatuhumiwa kumtukana matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini) kupitia namba za simu (tunazihifadhi) ambayo inaaminika inamilikiwa na Mwisho Mwampamba.

Mwisho alipoulizwa na hakimu huyo alikana kutenda kosa hilo na Robert alipoulizwa kama ana ushahidi ndipo aliposema anao wa meseji hizo kwenye simu yake.

Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 11, mwaka huu huku Robert akitakiwa kufika mahakamani hapo na meseji hizo kama ushahidi.

Aidha, Hakimu Amina alisema dhamana iko wazi kwa mshitakiwa; mdhamini mmoja na shilingi laki 4 ambapo kaka mwingine wa Mwisho aliyezaliwa naye baba mmoja na mama mmoja, lsambe alimdhamini mdogo wake huyo.

NA Dustan Shekidele, RISASI mchanganyiko

Matusi yamlaza MWISHO MWAMPAMBA rumande

  • You'd think Rob would be grinning from ear-to-ear given he'd just popped the question..


Rob Kardashian and Blac Chyna have surfaced for the first time since revealing their shock engagement news earlier this week.

Given the pair seemed over the moon just the previous day, Rob struggled to raise a smile as they were seen out in Woodland Hills, California, on Wednesday.

Maybe it's because his family are still yet to publicly congratulate him?

The couple, who are set to wed after just three months of dating, had ditched their glam garms for laid back looks for the outing.

Mum-of-one Blac was showing off her curves dressed in leggings and a tight top, while Rob was displaying his slimmed down frame in a plain white T-shirt and blue shorts.

Blac, who was carrying an ice lolly in one hand, couldn’t resist flashing her huge new sparkler, raising the other hand to her glasses as she was snapped.

Their outing comes after Blac's baby father Tyga broke his silence on the bombshell news, saying he's happy for the pair while insisting he only wants her and their son King Cairo, three, to be happy.

Tyga, 26, tweeted: "Everybody deserves 2 be happy. What some1 does for their happiness is not my concern, as long as it's not interfering wit my happiness.

"It makes me happy to see the mother of my son happy.My only concern in this situation is my son. I want him in happy environments (sic).”

Blac, 27, was previously close friends with Rob's sister Kim Kardashian West but fell out with the family after Tyga started dating their younger sister Kylie Jenner, 18.

Meanwhile, Blac - who celebrated her engagement with Rob, 29, at a strip club - is excited to become a Kardashian.

Her representative told PEOPLE that the model, real name Angela White, is planning to use her given name once she ties the knot, saying: "She was more than excited, she was thrilled, just super happy.

"She’s soon to be Angela Kardashian. She’s ecstatic."

Rob Kardashian and Blac Chyna keep it low-key as they're seen for first time since engagement news


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Jumapili iliyopita alitoa simulizi ya enzi hizo akielezea jinsi baba yake mzazi alivyomnasa vibao kwa sababu ya kung’ang’ania shule.

Alisimulia mkasa huo wakati akizungumza na watu walioalikwa katika semina maalum ya kampeni iliyoitwa Mimi ni Nani, Shtuka Mapema iliyofanyika katika Ukumbi wa Josam House jijini Dar, ambako alisema baba yake hakusoma hata darasa moja wakati mama yake aliishia darasa la saba, lakini wote wawili hawakujua umuhimu wa elimu.

“Siku moja nilijifungia chumbani nikaanza kulia, mara baba akaja na kunikuta natoka machozi na makamasi, akaniuliza kwa nini nalia, nikamwambia nataka kwenda shule. Nililambwa makofi kwelikweli, sitasahau siku hiyo. Hii ni kwa sababu baba hakujua umuhimu wa elimu,” alisema Makonda.

Akaongeza: “Baba alitaka niwe mkulima wa nyanya kwa sababu siku hizo zao hilo lilikuwa na soko nchini Kenya lakini mama kwa upande wake aliunga mkono ndoto zangu za kusaka elimu.”

Akifafanua zaidi alisema,  kutokana na king’ang’anizi chake alifanikiwa kusoma hadi Chuo Kikuu na kuwa rais wa vyuo vikuu vyote nchini na kuleta mabadiliko makubwa kielimu kwani alitetea mambo mengi ya wasomi na yakafanikiwa.

“Hivi sasa baba nikimkatia tiketi ya ndege kuja Dar anasema nikatie ndege ya jioni ndiyo nzuri…” alisema Makonda na kusababisha ukumbi mzima kuangua kicheko. Aliwataka wasomi na watu wengine kutimiza ndoto zao badala ya kutegemea kuambiwa na watu au kusoma vitabu walivyoandika wenzao.

“Unajua kuna mtu aliyegundua umeme utokanao na maji lakini yupo mtu mwingine akakuna kichwa na akafikiri akaona kwa nini asitengeneze umeme kwa kutumia jua, akafanikiwa, mwingine akaona kwa nini asitengeneze umeme kwa kutumia makaa ya mawe, akajaribu na kufanikiwa… huu ndiyo ubunifu unaotakiwa,” alisema.

Katika semina hiyo wanasemina walihimizwa kufanyia kazi ndoto zao ambapo Kampuni ya Global kupitia kwa mwakilishi wao, Elvan Stambuli iliwaomba washiriki kucheza Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kwa kukata kuponi zinazopatikana katika magazeti ya Risasi, Uwazi, Amani, Wikienda, Ijumaa na Championi ili kujiongezea fursa ya kujishindia nyumba ya kisasa.

Na Elvan Stambuli, RISASI mchanganyiko

Maisha ni safari ndefu : Makonda asimulia alivyonaswa vibao