Angalia moja ya kazi ya WEMA aliyofanya na M-bebi wa IDRISA
Mwaka 2016 umeanza vizuri na kuwa wa neema kwa WEMA SEPETU na M-bebi wake IDRISA baada ya kuwepo wa tetesi kuwa Makampuni kama 3 hivi ya biashara zimeshajitokeza kutaka kumtumia mtoto wao anayetarajiwa kuzaliwa mwaka huu.
Wadau wa mjini wanasema kampuni hizo ambazo hadi sasa majina yapo kapuni inasemekana kuanza mazungumzo ya awali na Wema, imefahamika kuwa Makampuni hayo yana shauku kubwa ya kufanya biashara na mtoto huyo mtarajiwa maana wanahisi atakuwa kivutio kikubwa katika jamii kama walivyo wazazi wake. ( WEMA na IDRISA).
Inasemakana pia kuna baadhi ya maduka ya nguo yamejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kumvalisha mtoto huyo kwa mwaka mzima.....
Kama ilivyo ada Wema alitafutwa ili aweze kuthibitisha haya , kama kawaida yake alicheka na kudai atazungumzia habari hiyo muda muafaka ukifika ila kwa sasa hawezi kusema chochote “Kwa sasa ni mapema mno kuzungumzia hilo jambo, nitaweka wazi baadaye,” alisema Wema
No comments:
Post a Comment