MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani ambaye  ni mdogo wake Kim Kardashian, Khloe, amedai kwamba yupo tayari kuolewa tena na mume wake wa zamani, Lamar Odom.

Wawili hao walishafunga ndoa ila uhusiano wao uliingia dosari baada ya Lamar kujihusisha katika matumizi ya dawa za kulevya, hivyo mrembo huyo aliomba kupewa talaka lakini akasitisha mara baada ya kijana huyo kupelekwa hospitali baada ya kuzidisha madawa ya kulevya katika danguro na kupoteza fahamu Oktoba, mwaka jana.

“Naweza kusema sijui nini kinaweza kutokea siku ya kesho, lakini nimejifunza kwamba kama unataka kumchekesha Mungu mueleze mipango yako ya kesho.

“Nilikuwa kwenye uhusiano na Odom na nitaendelea kuwa naye daima bila ya kujali nini kimetokea, ninaamini chochote kinaweza kutokea, bado nina ndoto za kuolewa na yeye na atakuja kunioa tena,” alisema Khloe.

Mdogo wa Kim Kardashian aomba kuolewa na mume wake wa zamani kwa mara ya pili

No comments:

Post a Comment